Ijumaa 9 Oktoba 2026 - 13:24
Sheikh Naim Qassem Aipongeza Hawza ya Qum Kufuatia Kutuma Ujumbe wa Wanazuoni wa Hawza Nchini Lebanon

Hawza/ Katibu Mkuu wa Wapambanaji wa Hizbullah, Sheikh Naim Qassem, ametuma barua kufuatia ujumbe uliotumwa na Hawza ya Qum wa kuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya pili ya kuuwawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safi al-Din (quddisa sirruhuma), akitoa pongezi na shukrani kwa Hawza hiyo, mkurugenzi wake, wanazuoni, wafanyakazi wenzake na wanafunzi wote wa Hawza.

Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hezbillah nchini Lebanon, ametuma barua kufuatia ujumbe uliotumwa na Hawza ya Qum ili kuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya pili ya kuuwawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safi al-Din (quddisa sirruhuma), huku akitoa pongezi na shukrani kwa Hawza, mkurugenzi wake, wanazuoni, wafanyakazi wenzake na wanafunzi wote wa Hawza.

Katika ujumbe huo, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Naim Qassem amesema kuwa; Uislamu halisi wa Muhammad (s.a.w.w.), pamoja na kufuata njia ya Wilaya na uongozi wa Imam Khomeini (quddisa nafsuhu) na Imam aliyeuawa kkshahidi (quddisa sirruhu), vimezikutanisha Hezbullah na Hawza.

Amesema: “Leo hii, kutekeleza wajibu wa jihadi, mapambano ya muqawama, kuuwawa kishahidi na kujitolea chini ya bendera ya uongozi wa Walii wa Amri, Ayatullah Sayyid Mujtaba Hussein Khamenei (da'ma dhilluhu), baada ya kuuwawa kishahidi mashahidi wetu wenye thamani kubwa, ndilo jambo linalotuunganisha sisi na ninyi.”

Katibu Mkuu wa Hezbullah, akizungumzia vita viwili vya hivi karibuni, yaani vita vya “Uli al-Ba’s”, vilivyotokea baada ya kuuwawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah (quddisa sirruhu), na vita vya “Al-Asf al-Ma’kul”, vilivyotokea baada ya kuuwawa kishahidi Imam aliyeuawa kishahidi (quddisa sirruhu), amesema kuwa; Hizbullah iliingia katika vita vya pande zote dhidi ya uvimbe wa saratani wa utawala wa Kizayuni, pamoja na uhalifu na ukatili wake wote, na dhidi ya jeuri ya Marekani iliyokuwa nyuma yake, kwa kipindi cha miaka miwili.

Ameeleza kuwa; Hizbullah ilisimama imara na kuendeleza mapambano ya muqawama kwa kumfuata Imam Hussein (a.s.) na Bibi Zaynab (s.a.). Kwa neema ya Mwenyezi Mungu, iliweza kubatilisha mipango ya maadui, na itaendelea na njia hii ikiwa imesimama kidete, kwa heshima na fahari.

Katika kuendelea na ujumbe wake, Sheikh Naim Qassem alielezea matumaini yake ya kupata ushindi kamili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema kuwa wananchi wa Iran, vikosi vyake vya majeshi na viongozi wa serikali, wakiongozwa na Imam aliyeuawa kishahidi, pamoja na familia yake, wapiganaji wote, wanazuoni na makamanda, walipambana kwa nguvu zao zote na kusimama imara kama mlima.

Ameongeza kwa kusema:


«وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ»

“Na ilikuwa ni haki iliyo wajibu Kwetu kuwapa ushindi Waumini.”

Katibu Mkuu wa Hizbullah ametoa hakikisho kwamba Hizbullah itaendelea na njia hii kwa uthabiti na subira. Amesisitiza kuwa hakuna nguvu yoyote inayoweza kuitikisa Hizbullah, na kwamba kwa kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu, hakutakuwa na jambo litakalotokea isipokuwa uongofu, tawfiki na ushindi.

Mwisho wa ujumbe wake, Sheikh Naim Qassem ameeleza matumaini yake kwamba wote watakuwa miongoni mwa askari wa Imam wa Zama (ajjalallahu farajahu), kisha akatoa salamu zake kwa Hawza tukufu, kubwa na yenye kujitolea ya Qum, mkurugenzi wake, wanazuoni, manaibu wa mkurugenzi na wanafunzi wa Hawza hiyo. Pia, amemuomba Mwenyezi Mungu aijaalie ushindi wa mwisho kambi ya Muqawama.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha